Mlipuko wa bomu kwenye gari katika soko moja kwenye eneo la Washia, kaskazini mwa Baghdad leo umeuwa watu wapatao 50.
Mlipuko huo ulipiga katika eneo la soko huko Sadr City wakati wa pilika pilika za asubuhi. Maafisa wa afya na usalama wanasema wana wasi wasi kwamba idadi ya waliofariki dunia inaweza kuongezeka. Watu wapatao 40 walijeruhiwa katika shambulizi hilo.
Magari mengine kadhaa na majengo ya karib yaliharibiwa kwa kiasi kikubwa maafisa wanaeleza.