Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 09:27

Ghasia zazuka Iraq


Waandmanaji wanaoongozwa na kiongozi wa kidini wa kishiha Moqtada al-Sardi walikusanyika mbele ya jingo la bunge nchini Iraq kabla ya kuelekea katika eneo linalojulikana kwa shamra shamra.

Mji wa Baghdad uligubikwa na kujikuta katikati ya ghasia za kisiasa hapo jana, ambapo ilitangazwa hali ya hatari baada ya waandamanaji kuvamia sehemu za eneo ambalo limeshawahi kuitwa la kimataifa yaani “International Zone.”

Inaelezwa wabunge walikimbia na jeshi lipo katika hali kubwa ya tahadhari.

Mpaka Jumapili jioni, waandamanaji kwa muda walisimamisha harakati zao na kuanza kuondoka katika eneo hilo.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Sadr inasema hatua hizo zilifanyika kwa kutoheshimiwa ibada ya msafara wa kishiha.

XS
SM
MD
LG