Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:56

Misri yafanya mashambulizi ya anga Libya kulipiza kisasi


Miili ya wahanga wa shambulizi la Misri.
Miili ya wahanga wa shambulizi la Misri.

Misri imejibu shambulizi la silaha lililouwa dazeni ya Wakristo wa dhehebu la Coptic Ijumaa kwa shambulizi la angani lililolenga “vituo vya kigaidi” ndani ya Libya.

Vituo hivyo Libya vinaaminika ndiko ambako wapiganaji wa Kiislam waliokuwa na silaha na kutekeleza mauaji hayo walipata mafunzo yao.

Rais Abdel-Fattah el-Sissi ametangaza hatua za kulipiza kisasi katika hotuba yake kupitia televisheni masaa kadhaa baada ya watu wenye silaha waliojifunika nyuso zao waliposhambulia basi lililokuwa limebeba Wakristo wa dhehebu la Coptic wakivuka jangwa kuelekea jumba la makazi ya makasisi.

Maafisa wa Misri wamesema sio chini ya watu 28 waliuawa katika shambulizi hilo waliokuwa mikononi mwa watu hao wenye silaha.

“Shambulizi lenye maumivu makali limetekelezwa katika kambi hizo,” el-Sissi amesema, akikusudia sehemu hizo zilizolengwa na shambulio hilo la anga nchini Libya.

“Misri haitosita kushambulia kambi hizo za magaidi pahali popote,” amesema. Maafisa wa kijeshi wamesema kambi hizo zilizolengwa Libya zilithibitishwa kuwa na mafungamano na shambulizi hilo la basi, ambazo zinashukiwa kuwa nasikitiko na kikundi cha Islamic State.

Serikali ya Misri imesema kuwa washambuliaji wanaofika kumi wakiwa katika gari aina ya pickup walifanya mashambulizi kilometa 320 kutoka Cairo, wakitupa risasi kutoka katika silaha za aina ya machine-gunkulipiga basi lilokuwa limebeba mahujaji kwenda katika Makazi ya Makasisi nje ya mji katika jimbo la Minya ambako walikuwa wanakwenda kumuenzi Mtakatifu Samuel, ambaye ni padri wa karne ya saba. Watu wengine 25 walijeruhiwa.

This image released by the Minya governorate media office shows bodies of victims killed when gunmen stormed a bus in Minya, Egypt, May 26, 2017.

“Washambuliaji hawa walitumia silaha za automatiki,” gavana wa jimbo hilo Essam el-Bedawi amesema. Watizamaji wa televisheni walishuhudia picha za basi hilo, vioo vyake vyote vimevunjwa, na kuzungukwa na polisi na gari za kubebea wagonjwa.

Kulikuwa hakuna kikundi kilichodai kuhusika na shambulizi hilo, japokuwa inafahamika mafungamano ya kikundi cha Islamic State nchini Misri, ambayo yamefanya mashambulizi manne dhidi ya wafuasi wa dhehebu la Coptic tangia Disemba.

Shambulizi baya kuliko yote lilitokea Aprili 10, Jumapili ya Palm iliyoko kwenye kalenda ya kanisa la Coptic, wakati mabomu yaliporipuka katika makanisa yake mawili, yakiua watu 44 waliokuwa wakifanya ibada na kujeruhi zaidi ya watu 100.

Watu wa dhehebu la Coptic ni jamii kubwa kuliko zote za Wakristo katika mashariki ya kati. Wamekuwa kwa muda mrefu ni walengwa wa Waislamu wenye misimamo mikali, na kubaguliwa na Waislamu walio wengi katika nchi hiyo.

XS
SM
MD
LG