Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 06:36

Waumini 23 wa dhehebu la Coptic wauawa Misri


Watu wakipekuwa mabaki ya basi lililoshambuliwa wakati likiwa limebeba waumini wa dhehebu la Coptic nchini Misri.
Watu wakipekuwa mabaki ya basi lililoshambuliwa wakati likiwa limebeba waumini wa dhehebu la Coptic nchini Misri.

Maafisa wa Misri wanasema watu wenye silaha wameshambulia Ijumaa basi moja lililokuwa limewabeba waumini wa dhehebu la Coptic na kuwauwa watu wasiopungua 23.

Maafisa wanasema abiria 25 walijeruhiwa katika shambulizi hilo la leo.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kwamba kundi hilo lilikuwa linasafiri kuelekea katika makao ya watawa kusini mwa cairo.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani amesema watu wasojulikana wakiwa ndani ya magari matatu walisimamisha mabasi mawili na kuanza kuyashambulia kwa risasi.

Maafisa wa usalama wameanza msako wa kuwatafuta washambuliaji hao.

XS
SM
MD
LG