Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 16:16

Algeria yashinda Kombe la AFCON 2019 kwa kuichapa Senegal 1-0


Mashabiki wa Misri wakiwa makundi mawili katika uwanja wa mpira wa kimataifa wa Cairo, Ijumaa, 07.19.2019. Picha na Sunday Shomari.

Baghdad Bounedjah katika dakika za mwanzo aliipatia timu ya Algeria bao la ushindi katika Michuano ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON, 2019, Kombe la AFCON, Ijumaa, ambapo ilishiriki kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha miaka 29.

Algeria walipata ushindi wa bao moja kwa sifuri dhidi ya timu ya Senegal katika michuano ya finali hiyo iliyofanyika mjini Cairo.

Bounedjah alifanikisha mwanzo wa ndoto ya Algeria, katika dakika ya pili, golikipa wa Senegal Alfred Gomis aliyepitwa na mpira uliotinga katika nyavu ya goli lake.

Goli hilo lilitokana na mpira uliopigwa na Baghdad kumgonga mchezaji wa Senegal Salif Sane na kumpita nduki mlinzi wa lango la Senegal, Alfred Gomis.

Na hapo ndipo ilikuwa ni uthibitisho wa kutosha kwa mabingwa wa mwaka 1990 kuwa watachukuwa kombe katika mchezo wa ugenini kwa mara ya kwanza.

Rais wa muda wa Algeria Abdelkader Bensaleh naye aliwasili dimbani kushuhudia mchuano huo, jambo ambalo liliwapo moyo wachezaji wa timu yake.

Senegal, timu ambayo haijawahi kutwaa ushindi katika michuano ya AFCON walipewa penalti baada ya mchezaji wa Algeria kuunawa mpira lakini refa alibadilisha uamuzi huo.

Wachambuzi wanasema Senegal wakishiriki kwa mara ya pili katika fainali tangu 2002, walikuwa wakiwaelemea mahasimu wao katika kipindi kikubwa cha mechi.

Mchezo wa fainali kati ya Senegal na Algeria ulichezwa katika uwanja wa soka wa kimataifa wa Cairo, wakati uwanja ulifurika huku mashabiki mbali wakijitokeza kwa wingi kuja kuzishajiisha timu hizo.

Mwandishi wa VOA aliyeko Cairo amesema kuwa wakati wakiwa bado nje ya uwanja kuna mamia ya mashabiki waliokosa tiketi za kuingia uwanjani kwa sababu mpaka inafika jana tiketi zote zilishanunuliwa.

Mwanahabari huyo pia amesema akiwa jijini Cairo alipata kuzungumza na baadhi ya mashabiki waliokosa tiketi ambao ni raia wa Saudia Arabia.

Naye raia wa Misri aliefanikiwa kuingia kwa tiketi ya wadhamini, mapema masaa machache kabla ya mechi kuanza, shabiki huyo aliiambia VOA kwamba mashirika mengi ambayo ni wadhamini kwenye michuano hii walizinunua tiketi kwa wingi na kuzigawa mapema kwa watu mbali mbali wengi wao wafanyakazi wa mashirika hayo.

Ndani ya uwanja mashabiki ambao ni wananchi wa Misri waligawanyika makundi mawili wengi wao wakiishabikia timu ya taifa ya Senegal na waliosalia timu ya taifa ya Algeria.

Imetayarishwa na Waandishi wetu, Cairo, Misri

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG