Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 08, 2024 Local time: 14:17

AFCON 2019 MISRI : Viongozi wa chama cha soka Misri wajiuzulu


Mchezaj nyota wa Misri Mohamed Salah akionyesha kukata tamaa wakati wa pambano kati ya Misri na Afrika Kusini, katika uwanja wa mpira wa kimataifa wa Cairo Julai 6, 2019. Misri ilifungwa moja bila na Afrika Kusini (Photo by OZAN KOSE / AFP)
Mchezaj nyota wa Misri Mohamed Salah akionyesha kukata tamaa wakati wa pambano kati ya Misri na Afrika Kusini, katika uwanja wa mpira wa kimataifa wa Cairo Julai 6, 2019. Misri ilifungwa moja bila na Afrika Kusini (Photo by OZAN KOSE / AFP)

Rais wa chama cha soka cha Misri Hani Abou Rida amejiuzulu na kikosi kizima chaufundi kufuatia kutolewa kwa timu hiyo kusikotarajiwa katika michuano ya soka ya kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri.

Kwa mujibu wa AFP uamuzi huo ni wa kutimiza ni wa haki na wajibu ilisema taarifa ya chama cha soka nchini Misri baada ya kuwaangusha mashabiki. Akiongeza kwamba wajumbe wote wa bodi wameombwa kujiuzulu.

Matokeo ya mechi ya Jumamosi yalipelekea mshtuko mkubwa kwa mashabiki wapatao 75,000 katika uwanja wa Cairo pamoja na wananchi wa Misri kwa jumla wakishuhudia timu yao iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ikiangushwa kwa bao 1-0 na Afrika kusini.

Rida ameongoza chama cha soka cha Misri tangu tangu mwaka 2016, katika muda wote chama hicho kimegubikwa na misukosuko ikiwa ni pamoja na timu kutolewa mapema katiika michuano ya kombe la dunia 2018 katika hatua ya makundi.

Uwanja wa soka wa kimataifa wa Cairo uliokuwa umefurika watu na ngoma na matarumbeta yalikuwa kimya kabisa baada ya mchezo huo huku baadhi ya washabiki wakibubujikwa na machozi ya kutoamini kilichotokea.

Wengi waliduwaa na kutoka nje ya uwanja kwa muda wakiwa wanashangaa na wengine wachache wakimpigia makofi na kumtaja golikipa mahiri wa timu hiyo Ahmed El Shenawi anayechezea timu ya Al Ahly.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Sunday Shomari, Cairo, Misri

XS
SM
MD
LG