Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 00:58

Miguna asema 'afya yangu inazidi kutetereka'


Miguna Miguna akiwa Dubai

Wakili machachari Miguna Miguna anadai kuwa askari wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) wamekuwa wakijaribu kuingia kwa nguvu katika chumba ambako anashikiliwa katika uwanja huo wa ndege.

Dr Miguna amesema kuwa afya yake inazidi kutetereka.

Akizungumza na shirika la Habari la KTN siku ya Jumamosi usiku, jenerali wa kikosi cha harakati za upinzani kitaifa aliye jitangazia madaraka amesema watu wasiojulikana, wakisadikiwa kuwa ni polisi walikuwa wanajaribu kuvunja mlango ili kuweza kuingia ndani ya chumba chake.

Dr Miguna, ambaye alikataliwa kibali cha kuingia Kenya baada ya kushindwa kuonyesha pasi yake ya kusafiria ya Canada, ameendelea kudai kuwa watu ambao walikuwa wanajifanya wao ni madaktari walijaribu kuingia katika chumba hicho.

“Mtu ambaye alidai kuwa ni daktari alijaribu kuingia chumbani kwangu, nilimtaka athibitishe kama yeye ni daktari na alishindwa,” amesema.

Alipoulizwa wapi hivi sasa atakuwa anaelekea, alijibu: “ Sina hati za kusafiria. Nitaweza kusafiri pale tu nitapokuwa nina pasi yangu ya Kenya ambayo mahakama imeamrisha nirejeshewe bila masharti yoyote.”

Miguna amedai kuwa polisi huko UAE waliwazuia maafisa wa Ubalozi wa Canada walioko nchini Dubai kwenda kumuona akiwa katika chumba chake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG