Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilianza kwa kupoteza ushindi katika michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 baada ya Marcelat Sakobi kutolewa na mpiganaji masumbwi wa Ufilipino Nesthy Petecio katika pambano la wanawake Jumamosi Julai 24. Majaji wote watano walithibitisha kutolewa kwake baada ya shindano la raundi tatu kwa uzito wa Feather (54-57kg).
Endelea kuangalia pambano hilo katika picha...
#Olympics2020 #voaolympics : Michuano ya mchezo wa masumbwi katika Olimpiki Tokyo 2020
Mengue Ayissi Albert wa Cameroon alinyakua ushindi wake wa kwanza dhidi ya Dlamini Thabiso wa Swaziland katika pambano la uzito wa Welter (63-69kg) akipewa ushindi na majaji wote wanne.

5
Albert Mengue Ayissi wa Cameroon (Jezi nyekundu) na Thabiso Dlamini wa Eswatini

6
Albert Mengue Ayissi wa Cameroon (Jezi nyekundu) na Thabiso Dlamini wa Eswatini

7
Marcelat Sakobi Matshu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Jezi nyekundu) na Nesthy Petecio wa Ufilipino

8
Albert Mengue Ayissi wa Cameroon (Jezi nyekundu) akisheherekea ushindi wa pambano lake na Thabiso Dlamini