Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 16:30

Mahakama Mali yatoa adhabu ya fidia ya dola milioni 3.2 kwa mhalifu


Mji mkuu wa Timbuktu, Mali

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu imetoa amri kwa mtu mmoja mwenye msimamo mkali wa kiislam kulipa fidia ya dola milioni 3.2 kwa kuharibu masanamu ya kidini ya kihistoria ya miongo kadhaa huko Mali.

Al -Faqi al -Mahdi alihukumiwa na mahakama hiyo mwaka jana kwa kuharibu masanamu 9 na mlango wa msikiti wakiwa na silaha na matrekta makubwa.

Uhalifu huo ulitokea katika mji wa zamani wa kihistoria wa Timbuku, wakati wenye msimamo mkali walipochukua udhibiti kwa muda mfupi kaskazini mwa Mali mwaka 2012.

Katika maamuzi ya kihistoria mahakama iliamua uharibifu huo wa masanamu kuwa ni uhalifu wa kivita wakati ilipomhukumu Al -Mahdi miaka 9 jela.

Alikuwa anaweza kupata miaka 30 jela lakini mahakama ilifikiria kuhusu suala lake la kukubali makosa na kuonyesha kusikitishwa.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG