Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 00:42

Al-Shabab yapata pigo baada ya kiongozi kujiuzulu


Abu Mansur al-Amriki
Abu Mansur al-Amriki

Kiongozi namba mbili wa al-Shabab amesema amejiondoa katika kundi la wapiganaji hao lilio na makazi yake Somalia.

Mukhtar Robow, ambaye pia anajulikana kama Abu Mansour, alizungumza na vyombo vya habari katika hoteli mjini Mogadishu ambapo alitangaza hilo Jumanne.

“Napenda kusema kwa watu wa Somalia na jumuiya ya kimataifa kwamba nilijitoa kutoka katika kundi la al-Shabab miaka mitano na miezi saba iliyopita na sio mwanachama wa kundi hilo,” alisema katika tamko lilokuwa limeandikwa.

Amesema amejiondoa kwa sababu ya tofauti za kiitikadi.

“Nimejiondoa kwa sababu kumekuwa na kutokuelewana na tofauti za kiitikadi, jambo ambalo halina maslahi yoyote na dini, watu na nchi hii,” amesema.

Kiongozi huyo wa zamani wa al-Shabab amegusia kuwa anafanya mazungumzo na serikali ya Somalia na kusema “Nimatumaini yangu tunaweza kupata ufumbuzi wa amani ya kudumu.

XS
SM
MD
LG