Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:09

Mgonjwa wa Ebola mwengine agundulika DRC


Picha inayoonyesha kirusi cha Ebola
Picha inayoonyesha kirusi cha Ebola

Shirika la afya duniani-WHO limeeleza mtu mwengine amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC).

Vyanzo vya habari nchini DRC vimeeleza kuwa vipimo vya maabara vimethibitisha kuwa mtu huyo ameathirika na virusi vya Ebola wakati mlipuko wa ugonjwa unaendelea katika jimbo moja kaskazini mwa Congo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated press-AP, WHO imeeleza leo jumanne kwamba miongoni mwa kesi 20 zilizoshukiwa, kesi mbili zimethibitishwa kua ni virusi hivyo.

Ugonjwa wa Ebola unasemekana umesababisha vifo zaidi ya watu 11,000 huko Afrika magharibi katika kipindi cha mwaka 2013 na 2016.

Congo tayari imeshashuhudia milipuko saba ya ugonjwa huo. Watu watatu wamefariki katika jimbo la Bas-Uele huko Congo eneo lililopo zaidi ya kilomita 1,300 kutoka mji mkuu Kinshasa.

Hakuna tiba ya Ebola hadi hivi sasa, ni ugonjwa unaosambaa kwa njia ya maji maji mwilini kwa watu walioambukizwa. Chanjo mpya ya majaribio imeonesha kuwa na mafanikio dhidi ya virusi.

XS
SM
MD
LG