Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:10

WHO yathibitisha kuwepo Ebola DRC


Ramani ya DRC
Ramani ya DRC

Mtu mmoja amethibitika kuwa na ugonjwa wa Ebola baada ya kuchukuliwa vipimo huko kaskazini mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Msemaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa maafisa wake wametangaza mlipuko wa Ebola katika eneo la jimbo la Bas-Uele baada ya uchunguzi wa maabara kuthibitisha kuwepo kwa ugonjwa huo.

Msemaji wake, Christian Lindmeier, ameiambia VOA kwamba watu tisa katika eneo hilo wanaugua na imeelezwa kuwa ni homa ya Ebola.

Habari hizo zimeeleza kuwa watu watatu tayari wamefariki dunia.

WHO imesema kwenye akaunti ya Twitter kuwa inashirikiana na Wizara ya Afya ya Congo katika kudhibiti mripuko huo.

Wizara imesema katika tamko lake kwamba timu za madaktari, waratibu na wataalamu wameelekea katika eneo hilo na watawasili huko Jumamosi.

Mripuko wa ugonjwa wa Ebola mara ya mwisho ulitokea Kongo mwaka 2014 na kuua zaidi ya watu 40.

Ugonjwa huo ulizuka tena na kuathiri eneo kubwa la Guinea, Liberia na Sierra Leone mwaka huo na kuua watu zaidi ya 11,000.


XS
SM
MD
LG