Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 24, 2023 Local time: 16:27

Mgomo wa wafanyakazi wa makampuni ya magari Marekani waingia siku ya nne


Wafanyakazi wa kutengeneza magari Marekani wakishiriki mgomo wa kudai haki zao.

Mgomo wa wafanyakazi wa makampuni ya kutengeneza magari nchini Marekani, ambao ni wanachama wa muungano uitwao  United Auto Workers (UAW),  wanaopinga  makampuni matatu makubwa zaidi ya kutengeneza  magari ulifikia siku yake ya tatu Jumapili bila azimio lolote kutarajiwa.

Hata hivyo, mazungumzo ya muungano huo na kampuni ya General Motors (GM) yalikuwa yamepangwa kuanza tena.

Takriban wafanyakazi 12,700 wa UAW walishiriki mgomo katika viwanda vitatu, vinavyomilikiwa na Ford, Stellantis, na GM, mtawalia, katika hatua muhimu zaidi ya wafanyakazi wa viwanda nchini Marekani katika miongo kadhaa.

Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa muungano wa UAW kugoma kwa wakati mmoja dhidi ya watengenezaji magari wote watatu.

Muungano huo na makampuni hayo hawakuonekana kukaribia kufikia mkataba mpya, kufikia Jumapili, huku watengenezaji magari wakiahidi nyongeza ya takriban asili mia 20 katika pendekezo la kandarasi ya miaka 4½, ikijumuisha nyongeza ya asili mia 10 ya papo hapo. Vyama vya wafanyakazi vinadai nyongeza ya asili mia 40.

Rais wa UAW Shawn Fain aliliambia shirika la habari la MSNBC Jumapili kwamba maendeleo katika mazungumzo hayo yamekuwa ya polepole.

Mazungumzo kati ya muungano huo na makampuni ya Stellantis na Ford yalipangwa kuanza tena Jumatatu.

Forum

XS
SM
MD
LG