Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 05:38

Wafanyakazi wa kampuni kubwa za kutengeneza magari Marekani waanzisha mgomo wakiomba nyongeza ya mishahara


Wafanyakazi wa kampuni ya General Motors wakati wa mgomo wa muungano wa vyama vya wafanyakazi wa kampuni za kutengeneza magari, Septemba 17, 2019.

Muungano wa vyama vya wafanyakazi wa kampuni za kutengeneza magari hapa Marekani leo Ijumaa umeanzisha mgomo kwa wakati mmoja kwenye viwanda vitatu vinavyomilikiwa na General Motors, Ford na Chrysler vya mmliki Stellantis, na kuanzisha mgomo mkubwa wa wafanyakazi wa viwanda kwa miongo kadhaa.

“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Marekani, tutagoma kama wafanyakazi wa kampuni zote tatu kubwa,” Rais wa muungano huo unaojulikana kama UAW Shawn Fain amesema, akiongeza kuwa muungano wao utaendelea na mgomo huo kwa sasa, lakini hatua zaidi zitachukuliwa ikiwa hakuna makubaliano juu ya mikataba mipya.

Kumekuwa na mivutano kwa wiki kadhaa kati ya Fain na wakurugenzi wakuu wa kampuni hizo tatu juu ya maombi ya muungano huo kupewa mishahara mikubwa kutokana na mapato ya malori yanayotumia mafuta, kuhakikishiwa kwamba wafanyakazi hawatapoteza ajira wakati kampuni hizo zimejikita katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme.

Mgomo huo ulibadilika kuwa suala la kisiasa, huku Rais Joe Biden, ambaye anawania muhula wa pili mwaka ujao, akitoa wito wa kufikiwa makubaliano.

Forum

XS
SM
MD
LG