Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:38

Mgombea urais wa zamani Uganda awania kuwawakilisha wazee bungeni


Jengo la Bunge la Uganda, Kampala, Sept. 28, 2017.
Jengo la Bunge la Uganda, Kampala, Sept. 28, 2017.

Aliyekuwa mgombea wa urais na waziri wa habari na mawasiliano nchini Uganda Aggrey Awori, ameteuliwa kuwania nafasi ya kuwakilisha wazee katika bunge la taifa.

Aggrey mwenye umri wa miaka 80, ambaye ni kaka ya aliyekuwa makamu wa rais nchini Kenya Moody Awori, atawakilisha wazee, kutoka Kijiji cha Madibira B, manispaa ya Busia.

Nafasi ya kuwakilisha wazee imeundwa hivi karibuni na bunge la Uganda, ili kuwa na watetezi wa maslahi ya watu hao katika sheria za nchi hiyo

Aggrey Awori, alikuwa mbunge wa Samia Bugwe kaskazini. Aligombea urais mwaka 2001 na kumaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Yoweri Museveni na Dkt Kiiza Besigye.

Awori amesema kwamba lengo lake bungeni litakuwa kupigania maslahi ya wazee hasa kuongezewa pesa wanazopokea kila mwezi kutoka serikalini, kutoka shilingi 25,000 hadi 100,000.

Anataka pia wazee wapatiwe matibabu bila malipo na haki yao ya kumiliki mali hasa ardhi kuheshimiwa.

Baadaaye alijiunga na chama cha National resistance movement NRM kutoka chama cha Uganda Peoples Congress – UPC.

Aligombea kiti cha bunge mwaka 2011 kwa mara nyingine lakini akapoteza kwa mgombea wa chama cha upinzani FDC.

XS
SM
MD
LG