Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 16, 2025 Local time: 17:41

Meli ya mizigo iliyoshambuliwa bahari ya Shamu iko hatarini kuzama


Meli ya mizigo ikiwa katika habari ya Shamu huko Yemen November 22, 2023 na AFP
Meli ya mizigo ikiwa katika habari ya Shamu huko Yemen November 22, 2023 na AFP

Huku hayo yakijiri, Waasi wa Houthi wa Yemen walilenga meli ya mizigo ya Rubymar katika Ghuba ya Aden na sasa iko katika hatari ya kuzama, kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la kundi hilo Yahya Sarea kupitia taarifa yake Jumatatu

Meli hiyo ni ya Uingereza na wafanyakazi wako salama, alisema, akiongeza kuwa wa Houthis pia wameiangusha ndege isiyo na rubani ya Marekani huko Hodeidah.

Meli ya mizigo inayosafiri kwa kutumia bendera ya Belize, iliyosajiliwa Uingereza na inayoendeshwa na Lebanon ilishambuliwa katika Mlango wa Bab al-Mandab karibu na Yemen Jumapili (Februari 18), kampuni ya usalama ya baharini ya Uingereza ya Ambrey ilisema.

Shirika la Operesheni za Biashara ya Baharini la Uingereza liliripoti kuwa wafanyakazi walikuwa wameiacha meli kutoka Yemen baada ya mlipuko

Forum

XS
SM
MD
LG