Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 30, 2022 Local time: 05:21

Mchunguzi wa biashara ya pembe auwawa Kenya


Pembe za ndovu zilizokamatwa zikiwa katika mchakato wa kuziharibu.

Mmoja wa wachunguzi wa juu kuhusiana na biashara haramu ya pembe za ndovu na za faru ameuawa nchini Kenya.

Esmond Bradley Martin alikutwa nyumbani kwake mjini Nairobi jana jumapili akiwa na jeraha la kuchomwa kisu shingoni.

Mmarekani huyo mwenye umri wa miaka 75 alikuwa akijulikana kwa kazi ya uchunguzi ambayo ilipelekea kuwabainisha wasafirishaji pembe na masoko ya biashara hiyo haramu.

Mkuu wa Wildlife Direct, Dr Paula Kahumbu amesema utafiti wa Martin ulipelekea kuibua biashara ya pembe nchini Marekani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vietnam, Nigeria, Angola, China na hivi karibuni Myanmmar.

Kazi yake ilikuwa muhimu sana kwa uamuzi wa China kuacha biashara haramu ya pembe za faru mwaka 1993.

Utafiti wa Martin pia umepeleka china kuacha mauzo halali ya pembe za ndovu, na marufuku imeanza kutumika januari 01, 2018.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG