Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:18

Dennis Edwards aiaga dunia


Dennis Edwards
Dennis Edwards

Mwanamziki mashuhuri Dennis Edwards, miaka 74, ambaye alikuja kuwa mwimbaji maarufu ulimwenguni mwaka 1968 ameaga dunia Alhamisi iliyopita katika hospitali mmoja Jijini Chicago nchini Marekani.

Hata hivyo wakala wake Rosiland Triche Roberts hakutaja sababu za kifo chake.

Sauti yake Edward yenye kuvutia, ilivuma kwa miaka mingi akiimba mimbo ya kidini, na ilikuwa ni yenye kuzikonga nyonyo za wengi wapenzi wa muziki miaka ya 70.

“Marvin Gaye alikuwa rafiki yangu, na alikuwa akisema, “Mshikaji, natamani ningekuwa naweza kuimba kama wewe, kama ningekuwa na sauti ya kuvutia kama yako,” Edwards alisema hilo mwaka 2013.

“Na mimi nilimwambia, “ Mshikaji, unafanya utani? Mimi nataka kuimba kama wewe. Kila mtu anataka kufikia kiwango chako katika kuimba,”

Kabla ya kujiunga na bendi ya Temptations, Edward aliimba pamoja na kundi jingine la Motown, the Contours, waliovuma katika kibao chao maarufu cha mwaka 1962 “Do You Love Me” (kilichorikodiwa kabla ya kujiunga na bendi hiyo).

XS
SM
MD
LG