Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 05:16

Mbunge wa Chadema akamatwa akitokea matibabuni Afrika Kusini


Freeman Mbowe
Freeman Mbowe

Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee (CHADEMA), amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere International Airport (JNIA) Dar es Salaam akitokea nchini Afrika Kusini, alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Chadema Jumatatu imesema baada ya kukamatwa Jumapili alfajiri alipelekwa kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Central Police).

Mpaka mchana wa Jumatatu Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia Katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na hajapatiwa dhamana pamoja na daktari wake kuwathibitishia polisi kuwa Halima ni mgonjwa, imeeleza taarifa hiyo.

Tunasikitishwa na kulaani kitendo hiki cha Polisi kuendelea kumshikilia mgonjwa ambaye alikuwa amelazwa hospitalini, imeeleza taarifa ya Chadema.

Taarifa hiyo imesema: “Tunatoa mwito kwa Jeshi la Polisi limpatie dhamana ili aweze kuendelea na matibabu yake, kwani dhamana ni haki yake na zaidi ni kuwa huyu bado ni mtuhumiwa na ni Mgonjwa ambaye ametoka matibabuni.

Wamesema mwisho wa yote Jeshi la Polisi litawajibika kwa watanzania endapo afya ya Halima Mdee ikitetereka au ikidhoofu zaidi na lawama zote zitakuwa juu yao.

Mdee pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe walitakiwa kuwa wanaripoti Polisi kwa amri ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambapo Jumanne tarehe 27 Machi hakuambatana na wenzake waliofikishwa mahakamani siku hiyo.

XS
SM
MD
LG