Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa bingwa wa dunia wa Olympiki Asbel Kiprop aliwaongoza Wakenya wengine Nzisa, Chepkoech na Koros kutwaa dhahabu hiyo katika shindano maalum la "Mixed Relay."
Hii pia ni mara ya kwanza kuandaliwa shindano la kupokezana vijiti katika mbio za dunia za Cross Country.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na shirikisho la kimataifa la riadha - IAAF yamerejea Afrika Mashariki baada ya miaka Kumi.
Kabla ya Uganda kukabidhiwa fursa ya kuwa mwenyeji mwaka huu, Kenya iliandaa mashindano hayo katika mji wa Mombasa mwaka wa 2007.
Imeandaliwa na mwandishi wetu Josephat Kioko, Kenya