Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 20, 2024 Local time: 03:39

Mazungumzo ya kufufua mkataba wa Nyuklia wa Iran yaahirishwa


Mkuu wa ujumbe wa Iran, Abbas Araghchi akiondoka katika Hoteli ya 'Grand Hotel Vienna' ambapo mkutano wa faragha wa nyuklia unafanyika Vienna, Austria, Jumamosi, Juni 12, 2021. (AP Photo/Florian Schroetter)
Mkuu wa ujumbe wa Iran, Abbas Araghchi akiondoka katika Hoteli ya 'Grand Hotel Vienna' ambapo mkutano wa faragha wa nyuklia unafanyika Vienna, Austria, Jumamosi, Juni 12, 2021. (AP Photo/Florian Schroetter)

Mazungumzo kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ili kufufua tena mkataba wa nyuklia wa 2015, yameahirishwa Jumapili ili kuwapa nafasi wajumbe kurudi katika miji mikuu yao kwa mashauriano.

Mkuu wa ujumbe wa Iran Abbas Araqchi anasema uamuzi huo uliyochukuliwa kwa sababu tofauti zilizobaki hazijaweza kutanzuliwa kwa urahisi.

Anasema hivi sasa wako karibu zaidi kufikia makubaliano kuliko wakati mwengine lakini tofauti kati yao kuweza kufikia mkataba ni ngumu kutanzua na wanahitaji kurudi nyumbani kupata ushauri zaidi.

Haijafahamika bado mazungumzo hayo yata anaza tena lini, kutrokana na kwamba mwanaisiasa mwenye itikadi kali za kihafidhina, Ebrahimi Raisi alipata ushindi kwenye uchaguzi wa Ijumaa akichukua nafasi ya rais mwenye msimamo wa wastani Hassan Rouhani.

Mabadiliko hayo hata hivyo hayatabadili juhudi za hivi sasa za kiongozi mkuu wa kidini Ayatollah Ali Khamenei mwenye sauti ya mwisho kuhusu sera muhimu za taifa hilo, za kufufua mkataba wa nyuklia na kuondolewa kwa vikwazo vikali vya mafuta na fedha vya Marekani vilivyodumaza uchumi wa Iran.

Majadiliano yamekuwa yakiendelea mjini Vienna tangu mwezi April kutafuta njia ambazo Marekani na Iran zinabidi kuchukua juu ya shughuli za nyuklia na kuondolewa vikwazo ili kurudi katika kutekelezwa kikamilifu mkataba wa nyuklia.

XS
SM
MD
LG