Maziko ya mapacha hao yamehudhuriwa na watu wengi ambao walijitokeza kutoa heshima zao za mwisho.
Vyombo vya habri vimeripoti kuwa kati yao ni viongozi wa madhehebu mbalimbali na serikali. Pia Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako alikuwa ni miongoni mwa viongozi hao.
Askofu wa Jimbo la Njombe, Kanisa Katoliki, Alfred Maluma amesema vifo vya mapacha hao vitumike na wananchi katika kukumbushana jukumu lao katika kuwalea watu wenye ulemavu.
Marehemu hao walizikwa katika makaburi ya Tosamaganga baada ya ibada ya maziko kufanyika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCU).