Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 30, 2023 Local time: 14:19

Mawakili Kenya wamshukia Rais Kenyatta


Majaji wa Mahakama ya Juu Kenya

Majaji nchini Kenya wamemtaka Rais Kenyatta kulinda haki ya majaji na idara yote ya mahakama badala ya kuwashambulia.

Chama cha Mawakili nchini Kenya (LSK) kimesikitishwa na kitendo cha Rais Uhuru Kenyatta kuwashambulia majaji wa mahakama ya juu kufuatia uamuzi wa kubatilisha uchaguzi wake.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimesema kuwa Rais wa LSK Isaac Okero alimkosoa Rais Kenyatta kwa kumtaja Jaji Mkuu David Maraga na majaji wengine wa mahakama hiyo kuwa wamekosea.

Rais Kenyatta ametoa matamshi hayo wakati wa ziara ya kukutana na wafuasi wake katika soko la Burma mjini Nairobi.

Hilo lilifuatia uamuzi wa mahakama hiyo ikiongozwa na jaji Maraga kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais.

Okero amesema matamshi ya rais kwamba majaji hao wasubiri rais achaguliwe katika uchaguzi ujao hayafai kutoka kwa kiongozi wa taifa ambaye chini ya katiba ya Kenya ni nembo ya umoja wa Wakenya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG