Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:36

Mauritius yasitisha safari za ndege na kuonya kuhusu kimbunga Freddy


Kimbunga Freddy kimepiga sehemu ya paa la jengo la Trou-aux-Biches, Mauritius, Februari 20, 2023. Reuters
Kimbunga Freddy kimepiga sehemu ya paa la jengo la Trou-aux-Biches, Mauritius, Februari 20, 2023. Reuters

Mauritius imesitisha safari za ndege na kufunga soko lake la hisa huku kimbunga Freddy kikikaribia kisiwa hicho kilichopo katika  Bahari ya Hindi siku ya Jumatatu, wakati timu za dharura zikijiandaa na mvua kubwa, mafuriko na maporomoko ya ardhi katika mikoa minne nchini Madagascar.

Kimbunga hicho, chenye upepo mkali wa kasi ya mpaka kilomita 120 kwa saa, ni tishio kwa Mauritius, kituo cha huduma za hali ya hewa cha kisiwa hicho kimesema

“Wakati kimbunga Freddy kinakaribia. Hali ya dhoruba inaweza ikasababisha mafuriko katika maeneo hatarishi ya pwani, kwa hiyo inashauriwa kuzingatia kutokwenda baharini, kituo hicho kimesema.

Video iliyothibitishwa na shirika la habari la Reuters ilionyesha upepo mkali na mawimbi yakipiga hoteli moja iliyoko ufukweni mwa bahari nchini Mauritius huku maji yakiingia kwenye ukumbi wa hoteli hiyo wakati wageni na wafanyakazi wakitazama.

Mamlaka ya kisiwa cha Madagaska kilichopo takribani kilomita 1,130 magharibi mwa Mauritius kuelekea pwani ya Afrika – imesema maeneo ya mashariki ya Mahanoro na kusini mashariki ya Manakara yanatarajiwa kukumbwa moja kwa moja na kimbunga hicho Jumanne jioni.

Chanzo cha habari hii kinatoka shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG