Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 04:30

Upelelezi Marekani unatafuta kichochezi cha mauaji ya Las Vegas


Rais Trump na mkewe Melania Trump wakielekea Las Vegas

Polisi wa Marekani hawajaweza kutambua vigezo vyovyote vilivyompelekea mshukiwa Stephen Paddock kufanya shambulizi la kinyama kwa risasi kwa watu wengi huko Las Vegas.

Shambulizi hilo lilipelekea kupotea maisha ya watu 59 na karibu 600 kujeruhiwa. Kaka wa mshukiwa anasema familia yao imeshtushwa kama watu wengine.

Ziara ya Trump

Rais wa Marekani Donald Trump amesema mashambulizi hayo ya Jumapili ni ukatili wa hali ya juu. Trump na Mkewe tayari wako njiani kuelekea Las Vegas Jumatano.

Baada ya tukio hilo Rais na Makamu wa Rais Mike Pence wakisindikizwa na wake zao, walitangaza kipindi cha ukimya Jumatatu mchana huko White House kwa heshima ya wale walioathirika. Rais pia aliagiza bendera za Marekani kupepea nusu mlingoti.

Shambulizi

Mshambuliaji huyo aliyetoboa shimo kwenye chumba cha hoteli yake na kupiga risasi kwenye kundi la watu waliojaa kwenye tamasha la muziki.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema waliposikia milio ya kwanza walifikiri ni baruti. Walipogundua ilikuwa ni risasi walipata mshtuko mkubwa.

Upigaji huo wa risasi huko Las Vegas ni mbaya kuliko wowote uliowahi kutokea wa shambulizi la mtu mmoja katika historia ya Marekani.

Polisi Shujaa

Miongoni mwa waliouwawa ni polisi aliyekuwa kwenye mapumziko aliyekuwa akisaidia watu kukimbia au kujificha.

Baada ya hapo watu walipanga foleni kuchangia damu. Mwandishi wa White amewasifu watu wa Marekani kwa hatua walizochukua baada ya tukio hilo.

Islamic State

Kundi la Islamic State limedai kuhusika na shambulizi hilo kupitia chombo chake cha habari, wakisema kwamba mshambuliaji huyo hivi karibuni alibadili dini na kuingia katika Uislam. Lakini wachunguzi hawakuweza kupata uhusiano wowote kati ya mshukiwa na kundi lolote lile.

Mkuu wa Polisi wa Nevada Joseph Lombardo amesema mtu huyu ni mshambuliaji wa peke yake, na amedadisi kuwa anashindwa kufahamu ni jinsi gani tukio hili lingeweza kuzuilika.

Shirika la Upelelezi FBI

Afisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) ambaye jina lake halikutajwa amesema hakuna uhusiano wowote uliothibishwa katika tukio hili na ugaidi wa ndani.

Familia ya mshambuliaji

Vyombo vya habari vimeeleza kuwa familia ya mshambuliaji huyu ilimuelezea kuwa mshambuliaji alikuwa mtu tajiri aliyependa kucheza kamari na kutuma zawadi za kifahari za vitafunwa kwa mama yake huko Florida. Lakini hakuwa na rekodi yeyote ya uhalifu.

Kaka wa mshambuliaji huyu Erick Paddock amesema: “Hii ilivyofanyika ni kama katupiga risasi . Nina maana angeweza hata kuuwa watoto wangu. Nimeshangazwa sana.

Hatua zinazopendekezwa

Shambulio hili la hivi karibuni linaleta majadiliano mapya juu ya nini kinaweza kufanyika kuzuia mauaji ya watu wengi bila kuingiza siasa. Wataalam wa ulinzi na usalama wanasema kukagua mabegi katika matamasha ya muziki ni njia mojawapo ya kuhakikisha hakuna mtu anaingia na bunduki.

Lakini katika hali ya mshambuliaji wa Las Vegas tayari alikuwa kwenye hoteli akiwa katika eneo la kuwapata vizuri watu waliojaa kwenye eneo lile.

Global Security

Mkuu wa shirika la Ulinzi Global Security David Katz amesema:“Uhalifu huu ni wa namna yake. Hakuna lolote ambalo lingeweza kufanyika kumzuia mtu kuchukua chumba kwenye hoteli katika eneo kama lile. Hili ni tukio lililokuwa baya sana.

Mshambuliaji huyo alijulikana kama Stephen Craig Paddock mwenye umri wa miaka 64 mstaafu kutoka Mesquite Nevada alikuwa na bunduki karibu 20 ikiwa ni pamoja na za kivita.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Sunday Shomari, Washington

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG