Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 13:03

Museveni na Besigye wachuana matokeo ya awali Uganda.


Rais Museveni akipokewa na wafuasi wake wakati wa kampeni.

Mgombea wa chama cha NRM nchini Uganda Yoweri Museveni anaongoza matokeo ya awali katika uchaguzi wa rais nchini Uganda kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliotolewa Ijumaa asubuhi na mwenyeiti wa tume ya Uchaguzi Dr. Badru Kiggundu.

Matokeo hayo yanaonyesha rais Museveni akiwa na kura 1,362,961 ikiwa ni sawa na asilimia 59, akifuatiwa na mgombea wa FDC Dr.Kiza Besigye mwenye kura 738,628 sawa na asilimia 36.8 na nafasi ya tatu ikiwa ni ya mgombea huru wa vugu vugu la Go Forward Amama Mbabazi mwenye kura 46,291 akifuatiwa na Abedi Bwanika ambaye mpaka sasa amejipatia kura 22,180 na Meja Jenerali Benon Rivami anazo kura 7,228.

Matokeo hayo ya awali yanaendelea kutolewa katika kituo cha kitaifa cha matokeo katika uwanja wa Namboole mjini Kampala Uganda.

Mwenyekiti wa tume Dr.Kiggundu hakueleza matokeo haya yanatokea maeneo gani .

Wakati huo huo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Dr.Kiggundu alitangaza alhamisi usiku kwamba vituo 14 vya Kampala vitarudia upigaji kura Ijumaa na vituo vingine 22 vya Wakisu, hii ni kutokana na kucheleweshwa kwa masanduku ya kura na matatizo mengine.

Matokeo haya ni asilimia 23 tu ya wapiga kura wa Uganda wanaokadiriwa kuwa milioni 15 .

XS
SM
MD
LG