Michuano ya 46 ya mbio Marathon kwa mwaka 2016 ilifanyika Jumapili katika jiji la New York Marekani ikishirikisha wanariadha wapatao 50,000 kutoka nchi 100 duniani.
Katika mashindano hayo walioshinda kwa upande wa wanaume ni Ghirmay Ghebreslassie wa Eritrea akitumia muda wa saa 2:07:51 na nafasi ya pili Lucas Rotich wa Kenya saa 2:08:53 na Abdi Abdirahman wa Mmarekani mwenye asili ya Somalia alishinda kwa saa 2:11:23 .
Na kwa upande wa wanawake Mary Keitany wa Kenya ameshinda medali ya dhahabu kwa muda wa saa 2:24:26 na nafasi ya pili imechukuliwa na Sally Kipyego wa Kenya aliyepata medali ya fedha aliyechukua saa 2:28:01 na nafasi ya tatu ilichukuliwa na Molly Huddle wa Marekani aliyechukua medali ya shaba kwa kutumia muda wa saa 2:28:13.
Mabingwa wawili wameshindwa kumaliza mbio za leo bingwa mtetezi wa michuano hii Stanley Biwott wa Kenya alishindwa kumaliza mbio hizo kutokana na maumivu ya misuli na mshindi wa Boston marathon 2015 Lelisa Dessisa wa Ethiopia pia alishindwa kutokana na maumivu ya msuli paja.
Mary Keitany wa Kenya ameweka rekodi ya kuwa mwanamke wa kwanza kushinda mashindano hayo mara tatu mfululizo tangu Grete Waitz kushinda mara tano 1982 -1986.
Bingwa wa dunia kutoka Eritrea Ghirmay Ghebreslassie, 20, ameweka rekodi ya kuwa mshindi wa Marathon ya New York mwenye umri mdogo zaidi.
Wakimbiaji wote wanaoshiriki michuano ya New York Marathon kuwa wanapewa namba maalum za kila mmoja wao ambazo mtu anaweza kumfuatilia ndugu yake kwa kutumia simu kama vile kifaa cha “GPS” cha kwenye gari.