Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 13:20

Marubani wa Kenya Airways wasitisha mgomo


Pilots of Kenya Airways strike, near the Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi
Pilots of Kenya Airways strike, near the Jomo Kenyatta International Airport in Nairobi

Chama cha Marubani wa Ndege nchini Kenya, KALPA, kimefuta notisi yao ya mgomo kufuatia uamuzi wa awali Jumanne wa mahakama ya ajira na Mahusiano, ambayo iliwaamuru marubani hao kurejea kazini.

Katika taarifa yake Jumanne usiku, KALPA ilisitisha notisi yao ya mgomo na kuwataka wanachama wao warejee kazini Jumatano kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.

Chama hicho kilisema kinajutia usumbufu ambao wateja wamepitia wageni wa KQ na kuwataka wanachama wao kurejesha hali ya kawaida mara moja.

Marubani hao walianza mgomo huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jumamosi, wakikaidi agizo la mahakama lililotolewa wiki jana dhidi ya hatua kama hiyo.

Hakimu wa Mahakama ya Mahusiano ya Kazi Anna Mwaure, Jumanne aliamuru "marubani wa Shirika la Ndege la Kenya Airways warejelee majukumu yao kama marubani bila masharti".

Shirika la ndege la Kenya Airways baadaye lilikaribisha uamuzi wa mahakama.

Waziri wa uchukuzi wa Kenya Kipchumba Murkomen alisema mgomo wa muda mrefu ungesababisha siyo tu kufungwa kwa shirika hilo ambalo lilikuwa likipoteza zaidi ya Sh300 milioni kwa siku, lakini pia kuathiri vibaya maisha ya zaidi ya 18,000 wanaotegemea shirika hilo.

Kesi iliyowasilishwa mahakamani na chama hicho cha marubani itaendelea kusikilizwa.

XS
SM
MD
LG