Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 07:25

Mgomo wa marubani wa Kenya Airways unakwamisha maelfu ya abiria


Marubani wa Kenya Airways wasitisha usafiri wa ndege na kukwamisha safari za abiria
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:34 0:00

Marubani wa Kenya Airways wasitisha usafiri wa ndege na kukwamisha abiria

Maelfu ya abiria wa shirika ndege la Kenya Airways wamekwama baada ya marubani wa shirika hilo kuanza mgomo siku ya Jumamosi asubuhi ulolazimisha kufutwa kwa mamia ya safari

Serikali ilijaribu kuwahimiza marubani wa moja wapi ya shirika kuu la ndege barani Afrika kutofanya mgomo wao, lakini inaonekana juhudi hazikufanikiwa.

Abiria wengi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi, wamewaambia waandishi habari kwamba hawakua na habari kuhusu mgomo huo hadi walipofika kuchukua ndege.

Lawrence Ndivo aliyekua anasafiri kwa ajili ya biashara, anasema aliarifiwa uwanjani kwamba safari imefutwa.

"Waliniambia nisiwe na wasi wasi niwasili kwa muda ulopangwa. Nilijisajilisha kupitia mtandao lakini nilipowasili hapa ndipo wameniarifu juu ya mgomo huu." alisema Ndivo

Shirika la marubani wa Kenya linasema wakurugenzi wa Kenya Airways walikata kusikiliza madai yao na mapendekezo ya namna kutanzua malalamiko yao kuhuiana na mishahara na malipo ya kustahafu.

Waziri wa usafiri Kipchumba Murkomen amewalaumu marubani kwa kutupa mazuri na mabaya kwa kutotanzua mabaya.

Akizungumza na waandishi habariJumamosi waziri amesema mgomo huo umesababisha abiria elfu 10 kukwama hadi hivi sasa. Aliongeza kusema ikiwa mgomo utaendelea basi utatahiri sektambali mbali za uchumi hasa utali .

XS
SM
MD
LG