Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 13:05

Trump amteua Mark Green kuongoza USAID


Green akizindua tafrija ya Shule ya Jitegemee alipokuwa balozi nchini Tanzania
Green akizindua tafrija ya Shule ya Jitegemee alipokuwa balozi nchini Tanzania

Jumuiya ya kimataifa inapumua baada ya Donald Trump kumchagua mwanadiplomasia mkongwe na mbunge wa zamani, anaye heshimika na wengi, Mark Green, kuongoza Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

Green ambaye ni balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania chini ya utawala wa George W. Bush na aliyekuwa Mwakilishi wa Wisconsin katika Bunge kwa mara nne.

Balozi huyu analeta uzoefu unaohitajika kwa Shirika ambalo linakabiliwa na punguzo kubwa la bajeti na mabadiliko makubwa, maafisa wa zamani wa USAID na wataalamu wa asasi binafsi wamesema.

“(Green) anafahamu kile kinachotakiwa kufanya misaada ya nje iwe na maana na kwa nini programu hizi ni muhimu sana kwa usalama wetu wa taifa na maslahi yetu ya kiuchumi,” amesema Liz Schrayer, Rais na Mkurugenzi mkuu wa shirika la US Global Leadership Coalition, mtandao wa asasi za kiraia wenye makazi yake Washington.

Iwapo atapitishwa na Baraza la Seneti, Green majukumu yake yatakuwa yamepungua. Morali ndani ya Shirika la USAID iko chini katika historia yake ikielekea katika mustakbali unaoyumba, baadhi ya maafisa wa zamani wa USAID na NGO wameiambia FP.

XS
SM
MD
LG