Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:28

Wanasiasa Marekani wadai uaminifu wa Trump uko mashakani


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump ataanza ziara yake ya kwanza ya kimataifa Ijumaa akielekea Mashariki ya Kati na Ulaya, bila shaka akiwa ameacha nyuma yake mtiririko wa kero za kisiasa ambazo zimeendelea kurindima kwa wiki nzima iliyopita.

Kero hizi zinafuatia hatua ya Trump kumfukuza kazi mkurugenzi wa FBI James Comey, kushutumiwa kutoa taarifa za siri kwa maafisa wa Russia, na repoti kwamba alimshinikiza Comey kusitisha uchunguzi dhidi ya aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa Michael Flynn ambaye anamafungamano na Russia.

Lakini katika vitu vyote ambavyo rais ataondoka navyo katika safari yake kikubwa ni ile shaka iliyoibuka juu ya uaminifu wake, jambo linalo kosolewa na Wademokrati na baadhi ya Warepublikan.

Mgogoro wa kisiasa lilikuwa wazi katika fikra za rais Jumatano wakati akitoa ushauri kwa wahitimu wa jeshi la majini la Marekani huko Connecticut waliomaliza mafunzo yao ya uofisa.

Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti limemtaka Comey kuhudhuria katika mahojiano ya siri na ya wazi, na mmoja wa viongozi wa Republikan, Mwakilishi Jason Chaffetz, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi ya Bunge, ameomba nyaraka zote ziletwe na mazungumzo yote yaliyo rekodiwaambayo yanatoa maelezo juu ya mazungumzo kati ya rais na Comey kabla ya kumfukuza kazi wiki iliyopita yawasilishwe.

Kufuatia mgogoro unaoikabili ikulu ya White House na maelezo yenye utata juu ya kufukuzwa Comey, Kiongozi wa Wademokrati katika Baraza la Seneti Chuck Schumer alikuwa anajiuliza wiki hii iwapo rais anaweza kuaminika.

“Kuna mgogoro tayari juu ya ukweli wa uongozi huu, ambao utatuumiza katika njia nyingi ambapo ni vigumu kuelezea kwa mapana yake,” Schumer amesema wakati akiwa katika ofisi za Baraza la Seneti.

“Juu ya yote hayo ni rais kutokuaminika na kupotea uaminifu wa nchi yetu kwa marafiki na washirika wetu.”

XS
SM
MD
LG