Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 07:05

Marekani yawawekea vikwazo Wataliban kwa "kukandamiza wasichana na wanawake"


Baadhi ya viongozi wa Taliban.
Baadhi ya viongozi wa Taliban.

Marekani ilitangaza vikwazo vipya Jumanne dhidi ya Taliban, kama adhabu kwa ukandamizaji wao wa wanawake na wasichana nchini Afghanistan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marakeni Anthony Blinken alitangaza vikwazo vipya vya visa kwa wanachama wa sasa au wa zamani wa Taliban, na wengine "wanaohusika katika kuwakandamiza wanawake kupitia sera na unyanyasaji."

Blinken alitoa tangazo hilo katika Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ya Umoja wa Mataifa.

"Kama mfano wa kusikitisha, kwa zaidi ya mwaka mmoja Afghanistan inasalia kuwa nchi pekee duniani ambako wasichana wamezuiwa kimfumo kuhudhuria shule baada ya darasa la sita, bila tarehe ya kurejea," Blinken alisema.

Baada ya kurejea madarakani mwezi Agosti 2021 kufuatia kuondoka kwa majeshi ya Marekani, kundi la Taliban lenye msimamo mkali limewazuia wasichana kuhudhuria shule za sekondari.

Hata hivyo, wanawake wanaruhusiwa kuhudhuria chuo kikuu.

Mlipuko wa hivi karibuni wa mjitoa mhanga kwenye darasa la shule moja mjini Kabul uliua na kujeruhi dazeni za wanafunzi walipokuwa wakijiandaa kwa mitihani.

XS
SM
MD
LG