Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:27

Taliban imemuachia huru Mark Frerichs wa Marekani


Mark Frerichs mateka raia wa Marekani aliyekuwa akishikiliwa na kundi la Taliban
Mark Frerichs mateka raia wa Marekani aliyekuwa akishikiliwa na kundi la Taliban

Taliban siku ya Jumatatu ilimuachia huru Mark Frerichs, mateka pekee wa Marekani aliyesalia nchini Afghanistan kwa kubadilishana na mbabe wa dawa za kulevya wa Taliban, Bashir Noorzai ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha maisha jela nchini Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa Taliban, Amir Khan Muttaqi amewaambia waandishi wa habari mjini Kabul kwamba kubadilishana wafungwa kati ya serikali yake na ujumbe wa Marekani kulifanyika katika uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Afghanistan.

Frerichs, mhandisi wa Marekani mwenye umri wa karibu miaka 60 na mkongwe wa jeshi la wanamaji, alitekwa nyara mjini Kabul mapema mwaka 2020 wakati wanajeshi wa Marekani na Jumuiya ya Kujihami ya NATO walipokuwa wakipambana na uasi wa Taliban wakati huo kuunga mkono serikali ya Afghanistan inayoungwa mkono na mataifa ya Magharibi.

Noorzai, maarufu kama Haji Bashir, alikamatwa mjini New York mwaka 2005 na hatimaye kushtakiwa kwa kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroin zenye thamani ya mamilioni ya dola nchini Marekani. Mshirika huyo wa ngazi ya juu wa Taliban aliripotiwa kusaidia kufadhili na kuwapatia silaha waasi hao mapato yatokanayo na biashara ya dawa za kulevya aina ya heroin.

XS
SM
MD
LG