Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 10, 2024 Local time: 04:12

Marekani yaonya wimbi la ugaidi linaloikabili Afrika


Mkuu wa AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, (Foto: Kantor Perdana Menteri Libya via Reuters)
Mkuu wa AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, (Foto: Kantor Perdana Menteri Libya via Reuters)

Mkuu wa kikosi cha Marekani kwa ajili ya Afrika Jenerali Stephen J Townsend ameonya wimbi la ugaidi linalolikumba bara la Afrika hivi sasa linabidi kushughulikiwa na dunia nzima.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi kubwa la pamoja la kijeshi kati ya wanajeshi wa Marekani, Afrika na Ulaya linalofahamika kama African Lion, mkuu wa Africom alipongeza kazi iliyofanyika mnamo wiki mbili za mazoezi lakini pia kutoa taswira ya vitisho vionavyojitokeza katika sehmu kadhaa za Afrika.

Jenerali Stephen J. Townsend, Mkuu wa Africa Command, katikati, akiwasili na Jeneral Belkhir el-Farouk, kulia, Kamanda wa Zoni ya Kusini ya Morocco, kushuhudia mazoezi ya ngazi ya juu ya kivita…
Jenerali Stephen J. Townsend, Mkuu wa Africa Command, katikati, akiwasili na Jeneral Belkhir el-Farouk, kulia, Kamanda wa Zoni ya Kusini ya Morocco, kushuhudia mazoezi ya ngazi ya juu ya kivita…

Jenerali Townsend amewaambia waandishi wa habari mjini Rabat ambako mazoezi yalimalizikia kwamba ana wasiwasi kutokana na hali ya usalama katika pembe mbali mbali za bara hilo kuanzia kanda ya Sahel upande wa Magharibi hadi Pembe ya Afrika.

Amesema mashambulio ya hatari yanayofanywa na makundi yenye uhusiano na Al-Qaida na Islamic State pamoja na wanamgambo wa al-Shabaab yanaendelea kuongezeka.

Mataifa jirani ya Afrika anasema yanasaidia serikali zinazokabiliwa na vitisho hivyo lakini anaongezea kusema juhudi hizo zote zinaonekana hazitoshi kusitisha kile anachokieleza ni “ Moto wa msituni wa ugaidi unaokumba bara hilo".

Zoezi la African Lioni liliwahusisha wanajeshi elfu 7 kutoka nchi saba pamoja na ushiriki wa NATO kwa kufanya mazoezi ya anga nchi kavu na bahari kwa pamoja huko Moroco, Tunisia na Senegal.

Vyanzo vya habari : AP na VOA News

XS
SM
MD
LG