Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:50

Biden atangaza mabalozi wapya watakaohudumu Israel, Mexico na NATO


Rais wa Marekani, Joe Biden

Majina yaliyotangazwa Jumanne na White House ni Thomas Nides, makamu mwenyekiti wa Morgan Stanley ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa mambo ya nje, chini ya Rais wa zamani Barack Obama atahudumu kama balozi wa Israel

Rais Joe Biden, Jumanne alitangaza wateule wake kuwa mabalozi wa Israel, Mexico na NATO wakati akiendelea kuimarisha ushirika wa Marekani katika maeneo magumu.

Miongoni mwa majina yaliyotangazwa Jumanne na White House, ni Thomas Nides, Makamu mwenyekiti wa Morgan Stanley ambaye aliwahi kuwa naibu waziri wa mambo ya nje, chini ya Rais wa zamani Barack Obama atahudumu kama balozi wa Israel. Mshirika wa karibu wa Marekani anaikaribisha serikali mpya baada ya bunge la Israel kumaliza miaka 12 ya utawala wa Benjamin Netanyahu kama Waziri Mkuu wa taifa la wayahudi hapo Jumapili.

Biden pia alimchagua Ken Salazar, seneta wa zamani wa jimbo la Colorado na waziri wa mambo ya ndani Marekani, kama balozi wake wa Mexico. Nchi hiyo ni moja ya marafiki wakubwa sana wa biashara na Marekani ambapo utawala wa Biden unafanya kazi kusimamia wahamiaji wanaokatisha mpaka wa Marekani na Mexico.

Mtalaamu wa usalama Julianne Smith alichaguliwa kuiwakilisha Maekani katika baraza la NATO.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG