Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 03:22

Marekani yamuua kiongozi wa Al-Qaeda, Ayman al-Zawahiri


FILE PHOTO: Picha ya aliyekuwa kiongozi wa Al-Qaeda Ayman al-Zawahiri
FILE PHOTO: Picha ya aliyekuwa kiongozi wa Al-Qaeda Ayman al-Zawahiri

Rais Joe Biden amethibitisha kwamba Marekani imemuua kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Ayman al-Zawahiri, katika operesheni ya maafisa wake wa kijasusi.

Akilihutubia taifa kutoka Ikulu mjini Washington DC Jumatatu jioni, Biden amesema kwamba operesheni ya kumtafuta al-Zawahiri ilikuwa imeendelea kwa muda mrefu, na kwamba aliidhinisha kuuawa kwake wiki jana.

Amesema mshukiwa huyo wa ugaidi alikuwa amejificha pamoja na familia yake katika nyumba moja mjini Kabul, Afghanistan, ambako aliuawa.

"Haki imetendeka. Kama wewe ni tishio kwa watu wetu, Marekani itakupata,” alisema Biden.

"Haijalishi itachukua muda gani, lakini tutakupata," aliongeza.

Al Zawairi, ambaye aliuawa siku ya Jumapili, alikuwa naibu wa mwanzilishi wa kundi la Al Qaeda, Osama bin Laden, na ni mmoja wa waatu walioshutumiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi hapa Marekani mwaka wa 2001.

Inaaminika kwamba alichukua uongozi wa kundi hilo baada ya kifo cha Bin Laden mwaka wa 2011.

Awali, afisa mmoja wa ngazi ya juu amesema Jumatatu kwamba Marekani mwishoni mwa wiki imefanya opereseheni isiyo ya kawaida ikilenga ngome ya al Qaida nchini Afghanistan akisema kwamba ilikwenda kama ilivyopangwa bila kuathiri raia wa kawaida.

Taarifa hiyo ilitolewa muda mfupi baada ya viongozi wa Taliban mjini Kabul kusema kwamba shambulizi la Jumapili kwenye makazi binafsi mjini humo lilifanywa kwa kutumia drone ya Marekani. Msemaji wa serikali ya Taliban ya Afghanistan Zibihullah Mujahid kupitia taarifa rasmi amekemea vikali shambulizi hilo , akiongeza kwamba opersheni hiyo ni kinyume na sheria za kimataifa inayokiuka makubaliano ya Doha pia.

XS
SM
MD
LG