Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 04:17

Marekani yaiomba serikali ya DRC kuwahami walinda amani wa UN


State Department spokesperson Ned Price
State Department spokesperson Ned Price

Marekani imeiomba serikali ya DRC kuwalinda walinda amani wa Umoja wa Mataifa na majengo yao kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo.

Maandamano ya kuipinga Tume ya UN nchini humo, inayojulikana kama MONUSCO, yamezuka tangu Jumatatu na kusababisha vifo vya watu 19 ikiwemo walinda amani wa UN watatu.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Ned Price amesema, Marekani inatoa wito kwa taifa na mamlaka za ndani za DRC kuhakikisha ulinzi wa MONUSCO, maeneo yao na wanajeshi na waandamanaji kujieleza kwa njia ya amani.

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Photo by Michel Lunanga / AFP)
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Photo by Michel Lunanga / AFP)

Marekani imesema mashambulizi dhidi ya maafisa wa UN na maeneo yao ni kinyume cha sheria za kimataifa na inashukuru nia ya dhati ya DRC kuchunguza vitendo hivyo.

XS
SM
MD
LG