Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 05, 2023 Local time: 10:18

Serikali ya DRC kuanza mnada wa vitalu 30 vya mafuta na gesi


Mto Congo unakumbana na uchafuzi unaosababisha athari nyingi.

Sehemu za msitu maarufu wa kitropiki katika Bonde la Congo ambao una jukumu muhimu katika mfumo wa hali ya hewa barani Afrika itauzwa kwenye mnada wa mafuta na gesi huko Kinshasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alhamisi.

Serikali ya DRC itapiga mnada vitalu 30 vya mafuta na gesi katika eneo la Cuvette-Centrale Peatlands katika msitu wa Bonde la Congo eneo kubwa zaidi la kitropiki duniani. Udongo wa msituni hujulikana kama eneo la kaboni kwa sababu iliyojaa ndani yake ni hifadhi kubwa ya kaboni ambayo hutolewa angani wakati mfumo wa ikolojia unapata matatizo.

Baadhi ya maeneo, au kambi, zilizowekwa alama za kukodisha mafuta ziko ndani ya eneo la kwanza la uhifadhi la Afrika, Hifadhi ya Kitaifa ya Virunga, iliyoundwa mwaka 1925 na eneo la Urithi wa Dunia la UNESCO, nyumbani kwa ngome ya mwisho ya sokwe wa milimani.

Bonde la Kongo lina ukubwa wa hekta milioni 530 katikati mwa Afrika na inawakilisha asilimia 70 ya ardhi yenye misitu ya bara hilo. Ina aina zaidi ya elfu moja za ndege na sokwe wengi zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote duniani, ikiwa ni pamoja na nyani wakubwa, sokwe na Bonobos.

Watu wako hatarini pia. Watu wa kabila la Mbuti na Baka huenda kufukuzwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG