Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 12:10

Marekani, Uingereza na washirika wa kimataifa wazindua mpango mpya wa usalama kwa Ukraine


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden huku Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg wakiwepo wakati walipohudhuria mkutano wa Baraza la NATO-Ukraine, Vilnius, Lithuania, July 12, 2023.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akiwa na Rais wa Marekani Joe Biden huku Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg wakiwepo wakati walipohudhuria mkutano wa Baraza la NATO-Ukraine, Vilnius, Lithuania, July 12, 2023.

Marekani, Uingereza na washirika wa kimataifa wamezindua mpango mpya wa usalama kwa Ukraine wakati  wa mkutano wa NATO hivi leo Jumatano.

Mpango huo umeandaliwa ili kuilinda nchi dhidi ya mashambulizi ya siku za mbele wakati Kyiv inajitahidi kuelekea kupata unachama wa muungano huo.

Matarajio ya ulinzi wa muda mrefu kutoka kwa wanachama wa muungano wenye nguvu wa kijeshi duniani yanakuja siku moja baada ya Rais Volodymyr Zelenskyy alilalamika kuwa si ‘vyema’ NATO kukataa kumpa ukaribisho au ratiba kwa Ukraine kujiunga na muungano huo.

Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg alifungua mkutano wa kwanza wa baraza la NATO na Ukraine hivi leo na kumkaribisha Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kama watu walio sawa.

Stoltenberg amethibitisha tena kwamba washirika wa NATO wamesimama pamoja na Ukraine katika , ‘mapambano ya kishujaa kwa ajili ya uhuru na utaifa.’

Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO anasema: “Bwana Volodymyr, tunasimama na wewe katika mapambano ya kishujaa kwa uhuru. Sisi tunawaangalia kwa unyenyekevu kwa kujitolea walikofanya Waukraine katika mapambano haya. Tumetiwa moyo na ushujaa wenu. Tunahitaji kuendeleza uungaji mkono wetu kuisaidia Ukraine kuikomboa ardhi yake na kuzuia mashambulizi ya siku za usoni ya Russia.”

Muungano una nia ya dhati kuipatia Kyiv msaada zaidi wa kijeshi kupigana na Russia lakini haijatoa muda maalum kuhusu uanachama wake.

Mpango huo ni sehemu ya juhudi za NATO kuileta Ukraine karibu na uwezekano wa kujiunga na muungano wa kijeshi bla ya kujiunga kiukweli. Jumanne, viongozi walisema katika waraka wao kuhusu mahitimisho ya kwamba Ukraine inaweza kujiunga ‘wakati washirika watakapokubali na masharti yametimizwa’.

Katibu Mkuu wa NATO anaongeza kuwa: “Katika mkutano huu, tumethibitisha tena kwamba Ukraine itakuwa mwanachama wa muungano, na tumefanya maamuzi ya kuileta Ukraine karibu na NATO. Leo tunakutana kama watu tulio sawa na ninasubiria siku ambayo tutakutana kama washirika.”

Akinyamaza kuhusu kusikitishwa kwake kutokana na kutokuwepo kwa ratiba ya kuwa mwanachama, Zelenskyy Jumatano alisema kuwa matokeo ya mkutano wa Vilnius yalikuwa mazuri kwa jumla na kukaribisha misaada mipya ya kijeshi kutoka kwa washirika.

Volodymyr Zelenskyy, Rais wa Ukraine anasema:“Tumejadili matarajio yetu kutoka katika mkutano wa NATO, na matokeo muhimu hapa ni kutambua kwamba Ukraine haihitaji ramani ya kuelekea kuwa mwanachama, katika njia hii, na pia nakushukuru tena, Jens kwa hatua hizi muhimu nafahamu kumekuwa na mwasiliano mengi tofauti na mikataba ambayo ilianyika, nashukuru sana kwa hili. Tumetoka mbali katika ushirikiano na NATO, na wanajeshi wetu wanafahamu vyema ushirikiano na wanachama mbali mbali wa muungano.”

Ukraine imekuwa ikisukuma kukubaliwa haraka kuwa mwanachama wa NATO wakati ikipambana na uvamizi wa Russia ulioanza February mwaka 2022 ambao umeua maelfu ya watu na kuwakosesha makazi mamilioni.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP

Forum

XS
SM
MD
LG