Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 25, 2024 Local time: 15:25

Zelenskyy anasema NATO lazima ithibitishe uanachama wa Ukraine


Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy

Ukweli wa usalama hapa kwenye eneo la mashariki la NATO unaitegemea Ukraine, Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya video wakati wa usiku. Tulipoomba kujiunga na NATO, tulikuwa wazi; Ukraine tayari iko katika muungano

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema NATO lazima ithibitishe uanachama wa Ukraine wakati wa mkutano wa siku mbili wa NATO huko Vilnius, Lithuania, siku ya Jumanne na Jumatano.

Ukweli wa usalama hapa kwenye eneo la mashariki la NATO unaitegemea Ukraine, Zelenskyy alisema katika hotuba yake ya video wakati wa usiku. Tulipoomba kujiunga na NATO, tulikuwa wazi; Ukraine tayari iko katika muungano. Silaha zetu ni silaha za muungano. Maadili yetu ni yale ambayo muungano unaamini. Vilnius lazima ithibitishe yote haya, alieleza.

Wanachama wa NATO wameendelea kugawanyika siku ya Jumatatu juu ya uwezekano wa Ukraine kuwa mwanachama katika muungano wa kijeshi kati ya wale wa Ulaya Mashariki na katika njia ya moja kwa moja ya uchokozi wa Russia ikiiunga mkono kuivamia Ukraine, na wale kama vile Marekani na Ujerumani wakihofia kuwa uanachama wa NATO kwa Ukraine kabla ya kumalizika kwa vita kutauingiza muungano mzima katika mzozo dhidi ya Russia na uwezekano wa kuchochea vita vya kimataifa.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg alisema amewasilisha mpango maalum ambao ulijumuisha kuondolewa kwa mahitaji muhimu ya kuingia kwa Ukraine katika muungano huo; Mpango wa Utekelezaji wa Uanachama (MAP) orodha ya malengo ya kisiasa, kiuchumi na kijeshi ambayo mataifa mengine ya Ulaya mashariki yalipaswa kukidhi kabla ya kujiunga na muungano huo.

Forum

XS
SM
MD
LG