Ripoti ya Klein ianeleza kwamba Msemaji wa White House Ray Carney siku ya Jumanne alitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu tukio la jumapili kama ilivyoelezwa na wizara ya ulinzi, Pentagon.
Kufuatana na maelezo haya, wanajeshi maalum wa Marekeani walipambana kwa risasi wakati wote wa operesheni hiyo iliyochukua takriban dakika 40.
Carney amesema, “ katika ghorofa ya kwanza ya jengo alokuwa anaishi Bin Laden, wasafirisha barua wawili wa al Qaida waliuwawa pamoja na mwanamke mmoja aliyeuwawa kutokana na risasi zilizokuwa zikifyetuliwa. Bin Laden na familia yake walipatikana katika ghorofa ya pili na ya tatu ya nyumba hiyo”.
Carney alisema Bin Laden alifanya upinzani wa kukamatwa na wanajeshi wa marekani wa Navy Seal walomvamia lakini hakuwa na silaha kinyume na maelezo ya awali. Akisema kukaidi kukamatwa haimanishi inahitaji mtu kuwa na silaha, lakini hakutowa maelezo zaidi.
Maelezo ya wizara ya ulinzi yalitofautiana pia na taarifa za awali zilzoeleza kwamba Bin Laden na washirika wake wengine waliwatumia wanawake kujificha kama kinga wakati wa mapigano.
Picha ya video ya uwaa ambako bin Laden aliuliwa
Msemaji wa ikulu Carney alisema “ Bin Laden na familia yake walipatikana katika ghorofa ya pili na ya tatu ya jengo hilo. Kulikuwa na wasi wasi kwamba huwenda Bin Laden akapinga operesheni ya kumkamata na kweli alikaidi. Ndani ya chumba pamoja na Bin Laden alikuwemo mwanamke, mke wa Bin Laden ambae alimvamia mwanajeshi wa marekani na alipigwa kwa risasi kwenye mguu lakini hakuuwawa. Baadae bin laden alipigwa risasi na kuuwawa. Hakuwa na silaha.”
Wakati huo huo katika mazungumzo yake na waandishi habari Jumanne, msemaji wa ikulu alisema, maafisa wanatafakari ikiwa watoe picha za Bin Laden baada ya kufariki kutokana na majeraha ya risasi kifuani na usoni.