Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 08:19

Marekani kutumia kifo cha Bin Laden kusambaratisha ugaidi


Rais Barack Obama(L) mwenye jaketi jeusi na timu yake ya usalama wa taifa wakifuatilia oparesheni ya siri iliyopelekea kuuwawa Osama bin Laden nchini Pakistan

Afisa wa cheo cha juu katika utawala wa Obama anasema Marekani inapanga kutumia kifo cha Osama bin Laden kuuharibu mtandao wake wa kigaidi wa al-Qaida.

Mkuu wa kupambana na ugaidi katika White House, John Brennan, alisema katika mahojiano na kituo cha televisheni cha NBC hapa Marekani katika kipindi cha Today leo Jumanne, kwamba kifo cha bin Laden kilikuwa ni mfululizo wa oparesheni za karibuni za Marekani ambazo zimepelekea kile anachokiita pigo kubwa kwa al-Qaida.

Pigo jingine kwa taasisi ya ugaidi linaweza kutokana na upelelezi uliokusanywa wakati wa tukio la kijasiri la uvamizi wa siri wa Marekani ambao ulimuuwa bin Laden mapema Jumatatu.

Maafisa wa Marekani wanasema wachambuzi wanaendelea kuangalia majalada na makaratasi ambayo kikosi maalum cha jeshi la majini la Marekani kilichukua kutoka kwenye nyumba yenye thamani dola milioni moja ambako mtu huyo aliyekuwa akitafutwa duniani alikuwa akiishi, kaskazini mwa mji mkuu wa Pakistan, Islamabad.

Waziri wa sheria wa Marekani, Eric Holder aliiambia kamati ya sheria katika bunge hii leo, kwamba ingawaje wa-Marekani wanaweza kujivunia oparesheni hii, taifa haliwezi kuridhika na hilo. Alisema mapambano dhidi ya ugaidi hayajakaribia kumalizika.

Wakati huo huo mwenyekiti wa kamati ya seneti ya uhusiano wa nje, mdemocrat John Kerry, alisema anapanga kusafiri kuelekea Afghanistan, katika kipindi cha chini ya wiki mbili kuzungumza na Rais wa Afghanistan Hamid Karzai na viongozi wengine juu ya kuuawa kwa bin Laden na namna hilo linavyoweza kuathiri baadhi ya shughuli zake.

Mkurugenzi wa idara ya ujasusi ya marekani, Leon Panetta amewaeleza wabunge katika barazala wawakilishi na seneti hii leo, juu ya kifo cha bin Laden.

XS
SM
MD
LG