Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Machi 23, 2025 Local time: 10:22

Trump atambua sera ya “China Moja"


Rais wa Marekani Donald Trump - Rais wa China, Xi Jinping
Rais wa Marekani Donald Trump - Rais wa China, Xi Jinping

Rais wa Marekani Donald Trump amemwambia Rais wa China Xi Jinping katika mazungumzo ya simu kwamba Marekani itaendelea kuheshimu sera ya “China Moja” kwa kutambua kuwa China ina mamlaka juu ya Taiwan pamoja na kujitawala.

White House imesema mazungumzo ya simu kati ya viongozi hao wa ulimwengu Alhamisi jioni yalikuwa ya “kirafiki” na pande zote “zimetoa mwaliko” kwa ajili ya kila mmoja kufanya ziara katika nchi ya mwengine.

Trump alikosolewa kwa kufanya mazungumzo ya simu na rais wa Taiwan mara tu baada ya kushinda uchaguzi wa urais Novemba mwaka jana.

Hakuna rais wa Marekani au rais mteule amewahi kuwa na mawasiliano kama haya na kiongozi wa Taiwan tangu Washington ilipovunja uhusiano rasmi na Taiwan mwaka 1979. Washington imekuwa ikiiunga mkono Taiwankwa njia isiyo rasmi.

Wakati wa makubaliano ya pamoja kati ya Marekani na China mwaka 1979, Marekani iliitambua Beijing kama ndio serikali halali ya China, ikikubali sera ya China ya "China mo" na Taiwan ni sehemu ya China.

Vyombo vya habari vya serikali ya China vimesema kutokana Trump kutokuwa na “uzoefu” kulimfanya akubali simu ya rais wa Taiwan, lakini wakaonya kuwa kitendo cha kuvunja sera ya China moja “kitaangamiza” mahusiano yaliyoko kati ya Washington na Beijing.

Trump alielekea kuingia matatani kutokana na majibu aliyopata kwa watu wa Marekani, akisema katika akaunti yake ya Twitter “inafurahisha jinsi Marekani inavyoiuzia Taiwan vifaa vya kijeshi vya mabilioni ya dola lakini mimi siruhusiwi kukubali pongezi kutoka Taiwan.”

Pamoja na China kupinga uamuzi huo, rais Barack Obama mwaka moja uliopita aliidhinisha kuiuzia Taiwan silaha za kujihami zenye thamani ya dola bilioni 1.83, zikiwemo manowari za kivita mbili, magari yanayoweza kupita majini na nchi kavu na silaha za kivita zinazoweza kupiga ndege na meli.

XS
SM
MD
LG