Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 13:03

Jubilee yasimamisha chaguzi za mchujo kaunti 47


Uhuru Kenyatta (kushoto), kiongozi wa muungano wa Jubilee na mwenzake William Ruto

Chaguzi za mchujo (awali) za Chama cha Jubilee nchini Kenya umesimama katika kaunti zote 47 kutokana na matatizo ya maandalizi, Katibu Mkuu Raphael Tuju amesema.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Tuju amesema siku ya Ijumaa kwamba baada ya mazungumzo na viongozi wa chama hicho, ilikubaliwa kuwa uchaguzi huo uahirishwe mpaka tarehe za baadae kuhakikisha uwazi na haki vinakuwepo katika chaguzi hizo.

Hapo awali Tuju alitangaza kusitishwa uteuzi huo katika kaunti za Narok, Kajiado, Kericho, Bomet, Uasin Gishu, Trans Nzoia, Baringo, Nakuru, Elgeyo-Marakwet, Nandi, Embu, Kiambu, Murang’a, Kirinyaga na Nyeri

Aidha chama cha Jubilee kilitangaza kuwa kitafuatilia kwa karibu upigaji kura katika kaunti za Murang’a, Kirinyaga, Nyeri na Nyandarua.

Katika kaunti nyinginezo, upigaji kura ulifutwa tu katika baadhi ya majimbo.

“Katika majimbo machache … maafisa wanaosimamia uchaguzi wataweza kufanya ziara ya mwisho.

Majimbo haya ni Laikipia, Meru na West Pokot,” amesema Tuju katika tamko lilotolewa baada ya kuzuka vurugu lilosabibishwa na ucheleweshaji na kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura vilivyoharibu mchakato huo.

Uchaguzi huo wa Mchujo wa Jubilee ulikumbwa na matukio kama vile kuchomwa moto kwa vifaa vya uchaguzi, maandamano ya wapiga kura katika kaunti mbalimbali, wakati kumekuwepo hofu ya uchakachuaji wa kura kwa upande wa wagombea na vitisho vya baadhi yao kuhamia vyama vingine.

Katika baadhi ya maeneo, Madaftari ya mwaka 2013 ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka yalikuwa yanatumika, yakiacha majina ya watu waliosajiliwa, na sehemu nyengine majina mengine ya wagombea hayakuwepo katika masanduku ya kupiga kura.

XS
SM
MD
LG