Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 18:07

Maporomoko ya tope yauwa Waganda


Maiti 18 zafukuliwa huko Bududa

Maafisa nchini Uganda wamesitisha operesheni ya kutafuta walionusurika katika maporomoko ya tope Jumatatu huku maiti 18 zikipatikana katika eneo la mlima Elgon mashariki mwa nchi hiyo. Lakini mpaka sasa watu wengi hawajulikani waliko.Waziri anayehusika na maswala ya majanga Stephen Malinga amesema Jumanne kuwa hamna uwezekano wa kupata watu walionusurika. Timu za wafanyakazi wa dharura zimepelekwa wilaya ya Bududa kufukua maiti ambapo pia watu mia 200 wamelazimika kuhama makazi yao. Mvua kubwa zilizonyesha kwenye eneo la mlima Elgon zilisababisha maporomoko hayo ya tope Jumatatu. Ibrahim Husssain mwalimu katika eneo hilo alisema wanafunzi walielezea kusikia mlio mkubwa wa sauti kabla ya miti na udongo kuanza kuporomoka.

XS
SM
MD
LG