Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:56

Mapinduzi ya haki za wafanyakazi yalianza Marekani


Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani nchini Kenya
Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani nchini Kenya

Shirikisho la Wafanyakazi nchini Marekani lilipitisha azimio kuwa ifikapo tarehe 1 Mei, mwaka 1886 na kuendelea masaa ya kazi yatambulike kisheria kuwa ni nane tu kwa siku nchini Marekani mwaka 1884.

Kufuatia azimio hili kuliibuka maandamano makubwa ya amani yaliyohusisha maelfu ya wafanyakazi ili kushinikiza waajiri na serikali kukubaliana na azimio hilo.

Hivi leo tunashuhudia sherehe za siku ya wafanyakazi karibuni ulimwengu kote.

Lakini kile ambacho tunasheherekea hivi leo kilikuja pamoja na wananchi kulipa thamani kubwa.

Kufanyika kwa maandamano kulipelekea viongozi wa wafanyakazi kukamatwa, kufungwa, kuteswa na baadhi yao kuuawa.

Lakini pamoja na matatizo haya yote wafanyakazi waliibuka kidedea kwani mwaka 1886 ilikubalika nchini Marekani kuwa saa za kazi ziwe nane tu kwa siku.

Mkutano mkuu wa pili wa kimataifa wa Jumuiya ya Wafanyakazi ulifanyika Paris Ufaransa mwaka 1890.

Mkutano huo ulipitisha azimio kuwa tarehe Moja Mei ya kila mwaka iadhimishwe duniani kote.

Hiyo ilikuwa namna ya kipekee ya kuwakumbuka wale walioteswa na kupoteza maisha yao wakipigania haki za wafanyakazi wenzao.

Lakini pamoja na juhudi zote hizo bado ziko nchi nyingi duniani ambazo bado watu wanakadamizwa na kunyimwa haki zao. Lakini bado kunamatumaini kuwa haki hizo zitafikiwa.

XS
SM
MD
LG