Usiku kucha, wale waliokuwa hawana mahema walilala ndani ya mablanketi chini, wakipika katika eneo la wazi kutokana na chakula cha msaada kilichogaiwa. Wengine walitengeneza mahema ya muda kutokana na mashuka yaliyofungwa kwenye miti, huku wengine wakisali wakiwa wamezungukwa na majengo yaliyoharibiwa na tetemeko.
Mmorocco aliyezaliwa Ujerumani Atik Azzouzi, mhandisi wa viwanda anayeishi Ujerumani, alikatisha likizo yake katika mji wa Nador ili kujitolea katika taasisi ya misaada ya Ujerumani kuja kuwasaidia wale wenye matatizo walioathiriwa na tetemeko la ardhi.
Waokoaji, wakisaidiwa na mbwa maalum, walipanda helikopta katika mji huo kuelekea kwenye zoezi jingine la uokoaji.
Waokoaji kutoka Uhispania, Uingereza na Qatar wanaendelea kuzisaidia timu za waokoaji wa Morocco, wakati Italia, Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani walisema misaada waliyoipendekeza inasubiri kuidhinishwa.
Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi lililokuwa la kiwango cha 6.8 kwa kipimo cha rikta lililopiga katika milima ya High Atlas Ijumaa jioni imeongezeka na kufikia 2,901, huku watu waliojeruhiwa wameongezeka maradufu na kufikia 5,530, televisheni ya serikali iliripoti.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.
Forum