Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:02

Makubaliano 'tete' kati ya Israeli na wanamgambo wa Islamic Jihad yaonyesha mafanikio


Mwanamke wa Kipalestina akitundika nguo alizoziokota kutoka katika kifusi August 8, 2022 nje ya nyumba yake, iliyoharibiwa kufuatia shambulizi la angani lililofanywa na Israeli wiki iliyopita huko mji wa Gaza, saa kadhaa baada ya kusitishwa mapigano.
Mwanamke wa Kipalestina akitundika nguo alizoziokota kutoka katika kifusi August 8, 2022 nje ya nyumba yake, iliyoharibiwa kufuatia shambulizi la angani lililofanywa na Israeli wiki iliyopita huko mji wa Gaza, saa kadhaa baada ya kusitishwa mapigano.

Sitisho la mapigano, ambalo lilianza rasmi kuanzia saa 11:30 (2030 GMT) Jumapili usiku, linalenga kumaliza mapigano mabaya kabisa huko Gaza tangu kumalizika vita vya siku 11 mwaka 2021 vilvyoharibu eneo la mwambao la Palestina.

Japokuwa mapigano na mashambulizi ya roketi yalifanyika wakati juhudi za kusitisha mapigano zikiendelea, huku ving’ora vikilia upande wa kusini mwa Israeli kabla na baada ya muda wa sitisho la mapigano, hakuna upande ulioripoti ukiukaji mkubwa wa makubaliano hayo baada ya saa nne kupita.

Katika taarifa iliyotumwa dakika tatu baada ya utekelezaji wa sitisho la mapigano kuanza, jeshi la Israel lilisema kuwa “ katika kujibu mashambulizi ya roketi yaliyorushwa kuelekea eneo la Israeli, (jeshi ) hivi sasa linashambulia maeneo mbalimbali” yanayomilikiwa na Islamic Jihad ndani ya Gaza.

Katika taarifa iliyofuatia, jeshi hilo lilifafanua kuwa shambulizi la “mwisho” lilifanyika saa 5:25 usiku.

Huku pande zote zikiwa zimekubaliana kusitisha mapigano, kila upande ulimuonya mwenzake kuwa itajibu kwa nguvu kwa ghasia zozote.

Rais wa Marekani Joe Biden alipokea kusitishwa mapigano kwa moyo mkunjufu, akimshukuru Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi kwa jukumu la nchi yake kusimamia makubaliano hayo. Biden pia ametaka uchunguzi ufanyike kutokana na kujeruhiwa raia, jambo aliloliita ni “msiba.”

Katika taarifa, mjumbe wa amani wa UN Mashariki ya Kati Tor Wennesland alisema: “Hali bado ni tete sana, na nahimiza pande zote kuendelea kuheshimu makubaliano yaliyofikiwa kusitisha mapigano.”

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP

XS
SM
MD
LG