Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 27, 2023 Local time: 14:26

Maktaba ya Congress Marekani kutunza 'tweets' maalum tu


Maktaba ya Bunge la Marekani

Maktaba ya Bunge la Marekani imesema kuwa haitaendelea kukusanya na kuhifadhi kila ujumbe wa tweet unaochapishwa katika akaunti za Twitter kama ilivyokuwa ikifanya kwa miaka 12 iliyopita.

Maktaba hiyo imesema wiki hii kuwa haina uwezo wa kukusanya kila kitu kinachotumwa katika mitandao ya kijamii kutokana na mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na kampuni ya Twitter, kwa kuruhusu ujumbe mrefu, picha na video.

Maktaba hiyo imesema katika blog iliyochapishwa wiki hii kuwa lengo lakini nambari moja katika kukusanya na kuhifadhi ujumbe wa tweet ilikuwa “ kuandika kumbukumbu ya jinsi mitandao ya jamii ilivyoibuka na kuendelea kukua kwa vizazi vijavyo.”

Maktaba hiyo imesema kuwa tayari imekwisha telekeleza lengo lake hilo na hakuna haja ya kuwa ni mkusanyaji “kina” wa ujumbe mbalimbali wa tweet.

Hata hivyo maktaba hiyo imesema itaendelea kukusanya na kuhifadhi ujumbe wa tweet siku za usoni, lakini itafanya kwa kuchagua kwa umakini zaidi baadhi ya tweet hizo.

Imesema kuwa hatua inayofuatia “ ujumbe wa tweet utaokusanywa na kuhifadhiwa utakuwa ni wa matukio au maudhui maalumu, ikiwa ni pamoja na matukio ya uchaguzi, au masuala ya maslahi ya kitaifa, kwa mfano sera za umma.”

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG