Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 19:47

‘Makamishna 4 wa IEBC walikuwa wakishirikiana na maafisa katika muungano wa Raila Odinga'


Makamishna 4 wa IEBC waliokataa kuidhinisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti nchini Kenya, wakiongozwa na makam mwenyekiti wa tume hiyo Juliana Cherera Aug 15,2022
Makamishna 4 wa IEBC waliokataa kuidhinisha matokeo ya uchaguzi mkuu wa Agosti nchini Kenya, wakiongozwa na makam mwenyekiti wa tume hiyo Juliana Cherera Aug 15,2022

Tume maalum iliyoundwa kuchunguza makamishna 4 wa tume huru ya uchaguzi nchini Kenya IEBC, imeambiwa kwamba makamishna hao walikuwa wanashirikiana na maafisa wa ngazi ya juu serikalini, na mkurugenzi mkuu wa muungano wa Azimio wa Raila Odinga, Raphael Tuju kulazimisha duru ya pili ya uchaguzi mkuu.

Makamishna hao wanachunguzwa kutokana na mwenendo wao baada ya kukataa matokeo ya uchaguzi wa urais yaliyompa ushindi William Ruto, namna yalivyotangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Tume hiyo imeambiwa kwamba kikao cha makamishna wanne wa IEBC kukataa matokeo ya uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti, waliochoandaa katika hoteli ya Serena jijini Nairobi, kililipiwa na watu waliokuwa na ushawishi mkubwa serikalini na katika muungano wa aliyekuwa mgombea urais Raila Odinga.

Vigogo katika muungano wa Raila Odinga walikuwa wakikutana na makamishna wa IEBC

Vile vile, walilipiwa hoteli ambapo walikuwa wanaishi na walikuwa wanafanya mikutano na mkurugenzi mkuu wa muungano wa Raila Odinga wa Azimio, Raphael Tuju pamoja na katibu mkuu wa chama cha KANU Nick Salat. KANU ni chama katika muungano wa Azimio.

Video ya CCTV inawaonyesha makamishna Juliana Cherera, Francis Wanderi, Justus Nyang’aya na Irene Masit wakiingia kwenye hoteli waliyokuwa wakiishi, wakitumia mlango wa nyuma ambapo magari yanaegeshwa.

Mfanyakazi wa hoteli hiyo Simon Ngila ameiambia tume ya uchunguzi kwamba alikuwa amepokea maagizo kutofuatilia zaidi kuhusu stakabadhi zao.

Tume hiyo imeambiwa kwamba kikao na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena kililipiwa na mtu anayeitwa Edwin Ng’ong’a Ongwe, kabla ya kuwalipia hoteli, na kwamba malipo yalifanyika saa mbili usiku, siku ambayo matokeo rasmi ya kura za urais yalitangazwa.

Makamishna walifichwa hotelini na kulipiwa

Ongwe, alikataa kusema watu waliokuwa wamepangiwa kuhutubia waandishi wa habari, na kuambia wafanyakazi wa hoteli kwamba walikuwa watu muhimu kabla ya makamishna wa IEBC kujitokeza na kuhutibia waandishi wa habari wakipinga matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yakitangazwa na mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Rekodi za hoteli zinaonyesha kwamba Tuju na Nick Salat walikuwa wakiwatembelea makamishna hao hotelini. Magari ya makamishna hao waliopewa na IEBC yalionekana katika hoteli waliyokuwa wanakaa

Mawakili wa makamishna hao hata hivyo wameelezea kukasirishwa na hatua ya kutolewa video ya makamishna hao kuonyesha mienendo yao na hata majibizano yakatokea wakati wa kikao.

Mkurugenzi mkuu wa IEBC Marjan Marjan, ameaimbia tume hiyo ya uchunguzi kwamba makamishna wawili kati ya wanne wanaochunguzwa; Irene Marsit na

Makamishna 2 kati yao walikuwa na jukumu la usamala wakati wa kutangaza matokeo

Francis Wanderi walikuwa wamepewa jukumu la kusimamia usalama katika ukumbi wa Bomas.

Vurugu zilitokea, baadhi ya watu walionekana wakiwa na rungu na maswali kuulizwa namna maafisa wa usalama walivyowaruhusu kuingia kwenye ukumbi huo na rungu.

Marjan vile vile amesema kwamba alishtuka kuona makamishna wanne wakihutubia waandishi wa habari katika hoteli ya Serena na kujitenga na matokeo ya kura za urais, wakati walikuwa wameshiriki katika kila hatua ya kujumulisha matokeo, hadi dakika ya mwisho, mshindi alipojulikana, matokeo yakionyesha kwamba kulikuwa na tofauti ya kura 233,000 kati ya Dr. William Ruto na Raila Odinga.

Marjan ameiambia tume hiyo kwamba Makamishna hao wanne walitaka tume kutangaza kwamba hakukuwa na mshindi, ili duru ya pili ya uchaguzi ifanyike, lakini mwenyekiti alikataa na kusema atatangaza matokeo namna yalivyokuwa.

Vikao vya uchunguzi vitaendelea mwaka ujao.

XS
SM
MD
LG